Home Habari za michezo KAGAME CUP KUANZA KINYONGE…SIMBA NA YANGA WASUSIA

KAGAME CUP KUANZA KINYONGE…SIMBA NA YANGA WASUSIA

HABARI ZA MICHEZO, SIMBA NA YANGA

PAZIA la mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) 2024 linafunguliwa leo ikiwa ni mara ya kwanza katika historia kwa mashindano hayo kufanyika Tanzania bila uwepo wa Simba na Yanga.

Tangu mashindano hayo yalipoanza mwaka 1967 yamefanyika Tanzania mara 19 na kati ya hizo, hakuna awamu ambayo Simba na Yanga zilikosekana kwa pamoja.

Simba ambayo ni bingwa wa kihistoria imetwaa mara sita na Yanga mara tano huku Azam ikichukua mara mbili, hazishiriki mashindano kwa kinachodaiwa ni kufanya maandalizi ya msimu ujao.

Kukosekana kwa timu hizo tatu, kumefungua milango kwa Coastal Union ambayo ilimaliza nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu Bara msimu uliomalizika na Singida Black Stars ambayo ilimaliza ikiwa ya saba kupewa fursa ya kuiwakilisha Tanzania Bara katika mashindano ambayo yanashirikisha timu 12 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nne kila moja.

Wawakilishi hao wa Tanzania Bara leo wote watakuwa kibaruani katika mechi za ufunguzi ambazo zitachezwa katika uwanja mpya wa KMC, Mwenge na Azam Complex ambavyo vyote vipo Dar es Salaam.

Mchezo wa kwanza utachezwa katika Uwanja wa KMC kuanzia saa 8:00 mchana ukihusisha mabingwa wa Ligi Kuu Zanzibar,, JKU dhidi ya Al Wadi ya Sudan. Saa mbili baadaye, Coastal Union itaingia uwanjani hapo kukabiliana na Dekadaha ya Somalia kanzia saa 10:00 jioni.

SOMA NA HII  4G ZA AZAM UJUMBE TOSHA KWA SIMBA