Home Habari za Simba Leo CHAMA AIFIKISHA SIMBA MAHAKAMANI…MADAI YA KIMKATABA

CHAMA AIFIKISHA SIMBA MAHAKAMANI…MADAI YA KIMKATABA

HABARI ZA YANGA-CHAMA

INAELEZWA kuwa kiungo mpya wa Yanga, Clatous Chama amefungua shauri kwenye mamlaka ya soka nchini akidai kuwa waajiri wake wa zamani hawajampa release letter ambayo itampa uhalali wa kuichezea Klabu ya Yanga.

Klabu ya Simba inaelezwa kuwa imekataa kumpa release letter ikidai aliondoka kinyume cha utaratibu kwenda Yanga.

Shauri hilo litasikilizwa leo 16 Julai 2024 pamoja na lile la Lameck Lawi mchezaji wa Coastal Union msimu wa 2023/24.

Lawi alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba kuwa ingizo jipya akitokea kikosi cha Coastal Union ambapo alikuwa hapo kwa msimu wa 2023/24.

Ndani ya ligi Lawi alicheza jumla ya mechi 25 akikomba dakika 2,230 alikuwa chaguo la kwanza kwenye benchi la ufundi la Coastal Union.

Baada ya kutambulishwa Simba, uongozi wa Coastal Union ulibainisha kuwa bado mchezaji huyo ni mali ya Coastal Union wanahitaji kuwa naye kwenye mashindano ya kimataifa ambapo Coastal Union inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Inaelezwa kwamba Yanga wamepanga kuweka kambi yao Avic Town kabla ya kusafiri na kwenda kushiriki mashindano waliyoalikwa Afrika Kusini.

Huko watacheza dhidi ya Kaizer Chief na klabu ya Bundasliga FC Augsburg ikiwa ni mechi za kirafiki.

Klabu ya Yanga hadi saa imetambulisha wachezaji wapya 5, ambapo Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka, Abubakar Khomeiny Mlinda mlango, na Kiungo Duke Abuya. na Azizi Andabwile.

SOMA NA HII  JOBE HUYOO ANASEPA...SIMBA KUMLIPA MIL 200