Home Habari za michezo BREAKING NEWS…STARTIMES KUONESHA LIGI ZOTE DUNIANI.

BREAKING NEWS…STARTIMES KUONESHA LIGI ZOTE DUNIANI.

Habari za Michezo Leo-Startimes

CHOMBO CHA HABARI-STARTIMES Julai 31, wamefanya mapinduzi makubwa ya Soka duniani, ambapo Meneja Masoko wa kampuni hiyo David Malisa aliweka wazi mpango kabambe wa kuonesha Ligi nyingi kubwa zilizopo Duniani.

Ligi ambazo zitakuwa zinaonekana kwenye Chaneli za Startimes ni Ligi Kuu ya Ujerumani Bundasliga, Michuano mikubwa zaidi ya Uingereza (Carabao Cup), Roshn Saudi League, LALIGA ya Yamal Lamine na Kylian Mbappe, Mashindano ya Copa Del Rey, na Ligi kuu ya NBC daraja la kwanza.

“Bila kusahau miaka yote, huu ni mwaka wa 8 tumekuwa tukionesha Ligi ya Bundasliga ambaye Shafii Dauda amekuwa akiitembelea Ujerumani yeye ataelezea kiukubwa zaidi, Ipo ndani ya Startimes, lakini pia kuna Ligi nyingine nyingi kama LALIGA, ROSHN SAUDI LEAGUE.

 

startimes zote ndani

“ZOTE NDANI maana yake zile Ligi zote kubwa pendwa unazipata ndani ya Kisumbuzi chako cha Startimes, lipia kifurushi chako mapema ili kutazama Ligi yako pendwa”

“Lakini leo nataka kuwaambia uanweza kuangalia Ligi zote kwenye kifurushi cha 17000, Sisi hatujabadilisha bei kama wale wengine, sisi tumeongeza thamani ya kuona mpira, na kwenda mabli zaidi unaweza kulipia kifurushi cha Wiki au cha Siku kama unataka kuangalia mechi ya Siku husika.” Davids Malisa- Mkurugenzi wa Masoko Startimes.

Nae kwa Upande wa Mkuu wa Kitengo cha Maudhui wa TV3 ndugu Skawa Jr alisema kuwa msimu huu watatoa maudhui yenye ubora mkubwa.

“Tumekuwa tunatoa huduma Bora kwenye matangazo lakini kwenye hili la ZOTE NDANI tutaongeza ubora na kufanya uchambuzi uliotukuka tukiwa na wachambuzi wabobezi kwenye soka” Skawa Jr.

 

Skawa Jr Startimes

Hafla hiyo ya Uzinduzi wa “ZOTE NDANI” ilihudhuriwa na Wachambuzi nguli wa Soka Nchini, Shafii Dauda, Amri Kiemba aliyewahi kucheza kwa mafanikio makubwa akiwa na Simba na Yanga, Priva Abiud Shaya, Privadinho, Tunu Hassan na David Kampista pamoja na waandishi wa habari na wadau wengine wengi.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AFUNGUKA JINSI SIMBA WALIVYOBADILISHA MBINU KATIKA MCHEZO WA JANA, CHANZO CHA SUB ZOTE ZILE NI HII