INAELEZWA kwamba Simba SC wako karibu na kumsajili mshambuliaji wa kati kutoka Cameroon, Leonel Ateba (25), yote yamehakikishwa.
Mchezaji huyo amevutiwa zaidi na Project ya Simba na yupo tayari kujiunga na Simba. Hakuna tatizo upande wake.
Kwa sasa, Simba na USMA wanafanya mazungumzo kuhusu ada ya uhamisho wa Ateba!
Awali, alicheza kwa Coton Sport, PWD Bamenda na Dyn. Douala na alijumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 27 wa Cameroon kwa ajili ya AFCON 2023.
Simba imelazimika kurudi sokoni haraka kutafuta mshambuliaji mwingine wa kumpa nguvu Steve Mukwala, ambaye muda mwingi amekuwa akiteseka kwa kuwasumbua mabeki lakini Simba inakosa mshambuliaji mwingine wa kutumia mipira inayoporwa na Mukwala.
Simba imecheza jumla ya dakika 180 bila washambuliaji wake kufunga bao hata moja, huku kwenye mechi hizo 3 wakiwa wamefunga mabao 3 sawa na wastani wa goli 1 kwa kila mechi.
Ujio wa Ateba unaiweka mashakani nafasi ya mshambuliaji wa sasa wa timu hiyo Fredy Michael Fungafunga.