Habari za Simba Leo
CEO FOUNTAIN GATES…KAGOMA TUMEMUUZA SIMBA…NAWASHANGAA YANGA
Abubakar
August 13, 2024
1:26 pm
CEO wa Fountain Gate FC (Zamani Singida Fountain Gate) amekiri kushangazwa na taarifa za Yanga kufungua kesi na kumuwekea pingamizi mchezaji Yusuf Kagoma
“Ni kweli Yanga ndio ilikua timu ya kwanza kabisa kuwasilisha Ofa ya kumuhitaji Kagoma na tuliikubali na walitanguliza Pesa kidogo
“Wakati wanafanya mazungumzo kuhusu maslahi binafsi ya mchezaji, Simba wakaingilia dili na mchezaji akaichagua Simba, Sisi kama klabu tukamuuza mchezaji alipotaka kwenda na tukawaeleza Yanga kwamba Kagoma ameichagua Simba
Yanga wakarejea tena wakataka Pesa walizotoa zihamishiwe katika uhamisho wa kiungo Aziz Andabwile na ndicho kilichofanyika na suala la Kagoma liliishia hapo
Sijui kwanini wameenda kulalamika TFF lakini kisheria Simba walifata taratibu zote na mchezaji ni mali yao halali”