habari za Simba- Awesu
Habari za Simba Leo

AWESU ARUDI SIMBA USIKU WA MANANE

Abubakar August 16, 2024 10:26 am

Klabu ya KMC imethibitisha kufikia makubaliano na Simba SC juu ya uhamisho wa mchezaji Awesu Ali Awesu ambaye awali KMC walimuwekea pingamizi kucheza Simba Sc kwa madai kuwa hakufuata taratibu za kuvunja mkataba.

Awali Awesu aliilipa KMC shilingi milioni 50 kama kipengele cha mkataba wake kilivyokuwa kinataka na kutangazwa kama mchezaji mpya wa Simba Sc.

Hata hivyo baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kupitia pingamizi la KMC wakabaini nyota huyo hakufuata taratibu za kuvunja mkataba na kuamriwa kurudi kwa Waajiri wake wa zamani kabla ya suala hilo kufikiwa muafaka leo.

Kwa mujibu wa taarifa ya KMC, makubaliano hayo yamefikiwa baada ya vikao vya timu zote mbili.

Inaelezwa Simba wameongeza dau la usajili  kutoka Mil 50 za awali na kutoa Milioni  20 nyingine,  hivyo dau la usajili la Awesu limefikia kiasi cha Tsh Milioni 70.

SIMBA YATUMIA MAMILIONI USAJILI WA ATEBA…MWENYEWE AFUNGUKA GAMONDI HATAKI MCHEZO…APIGA BITI ZITO KWA MASTAA WAKE