Home Habari za Simba Leo AWESU AWEKA NGUMU KMC…SIMBA YAONGEZA DAU LA USAJILI KUMBAKIZA

AWESU AWEKA NGUMU KMC…SIMBA YAONGEZA DAU LA USAJILI KUMBAKIZA

Habari za Simba- Awesu

KMC tayari wameshamtoa AWESU AWESU kwenye mipango yao kuelekea msimu ujao na Nahodha wao mpya ni KENNY ALLY MWAMBUNGU, kilichopo sasa kati yao ni kuwa wanahitaji Mchezaji aondoke ila kwa kufuata matakwa ya Kino Boys kwa mujibu wa mkataba.

KMC wapo tayari kufungua mazungumzo ya kumuuza Mchezaji endapo kuna klabu itakuwa tayari kulipa kiasi kinachoanzia MILLION 50, elewa hapo yani kama kuna klabu itakuwa tayari kulipa kuanzia kiasi hicho ndipo klabu ijulishwe na mazungumzo yaanze rasmi na ndio maana ya RELEASE CLAUSE.

SIMBA wapo tayari kuwapa KMC kiasi cha MILLION 70 yani ongezeko la MILLION 20 kutoka zile 50 za Kimkataba, lakini KMC wanataka biashara ianzie hapo hapo MILLION 200 na sio vinginevyo, huo ndio msimamo wa KINO BOYS mpaka sasa tunavyozungumza.

Taarifa nyingine ni kuwa KMC kufuatia mvutano huu hawakuweka mshahara wa Awesu wa mwezi JULAI baada ya Mchezaji kujitangaza kuwa amemalizana na KMC, bado libeneke linaendelea huku Mchezaji akisema hawezi kurudi KMC.

Taarifa nilizopata mpaka sasa ni kuwa Kiungo Awesu Awesu yupo kambini Mbweni kwa klabu ya Simba mpaka hivi sasa, huku mawasiliano kati ya Simba na KMC kufikia hitimisho juu ya suala la Mchezaji huyo bado halijafikiwa, taarifa ni kuwa mawasiliano yanasuasua huku mkazo wa KMC ukisalia ni MILLION 200.

Huku pia dirisha likifungwa rasmi hapo kesho AGOSTI 15, sakata hili bado halijapata ufumbuzi, msimamo wa Mchezaji ni kucheza Simba ama arejee visiwani kuendelea na mambo mengine yani akistaafu rasmi soka.

Ijapo vyanzo vyangu vinasema huenda jioni hii Viongozi wakubwa wa SIMBA na KMC watakutana ili kulimaliza rasmi jambo hilo, we are officially entering the final stages of this transfer saga.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUFANYA VIZURI....SIMBA HAWANA IMANI NA MGUNDA...KUMBE MPAKA SASA 'ANAPIGA DEIWAKA"...