Home Habari za Simba Leo SIMBA KUANZISHA CHANELI YAO YA KIARABU NA KIFARANSA

SIMBA KUANZISHA CHANELI YAO YA KIARABU NA KIFARANSA

HABARI ZA SIMBA LEO, MANGUNGU & MO

Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu amesema kwakuwa klabu hiyo inasafiri na kushiriki michuano mikubwa Afrika, wanatarajia kuanzisha chaneli mtandaoni.

Kwa lugha ya kiarabu na lugha ya kifaransa huku akisema kwenye bajeti ya 2024/2025 mitandao ya kijamii ya Simba inatarajiwa kuingiza Tsh. milioni 400.

Akiongea jana October 06,2024 kwenye Mkutano Mkuu wa Simba SC, Mangungu alisema;

“Tumezungumzia suala la digital platforms (kwenye bajeti ya 2024/2025 mitandao ya kijamii ya Simba inatarajiwa kuingiza Tsh. milioni 400), tuna mchakato unaoendelea, Timu yetu inasafiri na kushiriki michuano mikubwa Afrika, tunaanzisha chaneli kwa lugha ya kiarabu na lugha ya kifaransa”

“Sisi Bodi tutaunga utekelezaji wa mradi wa miundombinu, mwisho nitoe shukrani kwa serikali, tunasafiri Nchi mbalimbali na Maafisa wa Ubalozi wamekuwa wakija tunashirikiana ili kila kitu kwenda vizuri”

“Sisi Simba Sports Club tutaendelea kuunga mkono Serikali, tunafikia hatua ya mwisho ya mabadiliko lakini mabadiliko yoyote lazima yatakuwa na maumivu nadhani tuvumilie ili tumalize haya yote kwa pamoja”

“Tunamshukuru Rais wa Simba, Mohammed Dewji kwa hotub nzuri, pamoja na kusisitiza Wanachama na Wapenzi wa Simba kwenda viwanjani kuiunga mkono timu yao kadhalika tunawasisitiza sana umuhimu wa kutumia bidhaa zinazotokana na Wadhamini wetu”. Alisema Mangungu.

SOMA NA HII  NGEREZA AWALIPUA SIMBA......... LABDA YANGA LAKINI SIMBA HAWATOBOI