Home Habari za michezo KUELEKEA ‘DABI’…AHMED ALLY AWAPA TAHADHARI MASHABIKI WA SIMBA….

KUELEKEA ‘DABI’…AHMED ALLY AWAPA TAHADHARI MASHABIKI WA SIMBA….

HABARI ZA SIMBA

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa presha wanayokutana nayo kati ya Azam FC tofauti na Kariakoo Derby.

Amesema mechi hiyo dhidi ya Yanga wanatakiwa wanasimba wote kuungana na kuwa kitu kimoja katika siku ya Jumamosi, Oktoba 19 dhidi ya Yanga.

Katika mchezo huo Simba wanakuwa nyumbani kuwakaribisha Yanga katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam, saa 11:00 jioni.

“Hii mechi ya Jumamosi ni tofauti tunapokutana na timu kama Fountain Gate FC, Singida Black Stars na Azam FC ambao hao ni watoto wa 2000, tunakutana na mkubwa mwenzetu, mwanasimba wote wanatakiwa kuwa kitu kimoja.

Mwanasimba yoyote kuanzania sasa anatakiwa kuomba dua kwa imani yake kwa ajili ya mchezo huo wa utamaduni mkubwa na kugusa maisha yetu ya wanasimba,” amesema Ahmed.

Ameeleza kuwa sasa hawataki kuona wanapoteza mara nne katika mchezo wa Kariakoo Derby, wanatarajia kufanya vizuri kwa sababu ya kuwepo kwa kikosi imara na wachezaji kuwafurahish.

SOMA NA HII  WAKATI NCHIMBI AKITANGAZA KUONDOKA YANGA....UONGOZI WAIBUKA NA KUKANUSHA...WAFICHUA YANYUMA YA PAZIA...