Home Habari za michezo MWISHO WA MBAMBAMBA NI KESHO…ATAPIGWA MTU MPAKA ACHAKAE…

MWISHO WA MBAMBAMBA NI KESHO…ATAPIGWA MTU MPAKA ACHAKAE…

Vaibu la mashabiki wa Yanga na Simba limekolea kuelekea dabi ya Jumapili. Mastaa wa zamani wa Yanga wamedai mechi itamalizwa mapema kwa mtu kuumia na hakuna sare.

Wameviangalia vikosi vya timu hizo kwa uimara na udhaifu wao kisha kusema mechi hiyo haina sare tofauti na ilivyokuwa kwenye msimu uliopita kwani kuna timu itapasuka mapema tu.

Maka Edward, aliyewahi kukipiga Yanga alisema hakuna upande utakaokubali kufungwa kirahisi kutokana na mwendelezo wa sasa wa timu hizo katika ligi, akisema Yanga itakuwa na hasira za kutaka kupoza machungu ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Simba itakataa kuwa mteja Jangwani.

Maka anayekipiga kwa sasa JKT Tanzania iliyopo Ligi ya Championship, alisema kwa kasi waliyo nayo msimu huu watani hao yeyote anaweza kushinda na atakayejipanga vyema ndiye ataondoka na kicheko kwa Mkapa huku akisisitiza kuwa mabao yapo na mchezo huo hautaisha kwa sare.

“Mchezo utakuwa mgumu, ila suioni sare kabisa Jumapili, lazima mmoja ashinde kama sio Yanga basi ni Simba kutokana na namna kila moja ikitaka heshima mbele ya mpinzani wake,” alisema Maka aliyeichezea pia Geita Gold msimu uliopita.

Kwa upande wake, Abdi Kassim ‘Babi’, alisema ingawa Simba wako kwenye kiwango bora kwa siku za karibuni lakini hawapaswi kujiamini kupitiliza bali wanapaswa kuchukua tahadhari huku akiwaonya mashabiki wenye roho ndogo kutoweka matumaini makubwa wasije wakaumia baada ya dakika 90.

“Yanga uimara wao upo kati (kiungo) mpaka mbele (ushambuliaji), Simba uimara wao naona upo pembeni (winga) kwahiyo ni ‘game’ ngumu sana ila utakuwa mchezo mzuri wenye msisimko mkubwa na mshindi atapatikana ndani ya dakika 90,” alisema Babi aliye kocha msaidizi wa Mashujaa Kigoma.

Mechi hiyo ya watani ni moja ya karata muhimu kwenye mbio za ubingwa msimu huu kutokana na ushindani wa timu hizo kongwe nchini.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI