Home Habari za michezo ALIYEONA KIBABAGE AKIANGUKA GHAFLA UWANJANI AFUNGUA A-Z …..DAKTARI ATOA NENO HILI…

ALIYEONA KIBABAGE AKIANGUKA GHAFLA UWANJANI AFUNGUA A-Z …..DAKTARI ATOA NENO HILI…

Habari za Yanga leo

Beki wa kushoto wa Klabu ya Yanga, Nickson Clement Kibabage jauzi alilazimika kukimbizwa katika Hospitali ya Mount Meru, Arusha kwa ajili ya matibabu baada ya kuanguka ghafla uwanjani wakati mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ihefu ukiendelea.

Akizungumzia tukio hilo, mtangazaji wa mchezo huo ambaye alishuhudia tukio hilo, Gharib Mzinga amesema kuwa hakukuwa na mgongano wowote bali Kibabage alianguka tu peke yake uwanjani na kushika kichwa akiashiria kupata maumivu makali ya kichwa.

“Kibabage ali-collapse mwenyewe, hakukuwa na mguso, labda kama aliguswa mbali sana akaja ku-cllapse baadaye lakini alianguka mwenyewe. Picha za marejeo zilionesha alifanya marking, akashika kichwa akalala chini. Ndiyo maana uliona wachezaji wakiita madaktari kwa msaada haraka.

“Aliyeita madaktari ni wachezaji sio refa, fanyeni haraka kwa sababu matukio ya ku-collpase ni hatari. Madaktari wakaingia haraka na kwenda kuangalia tatizo ni nini na wakamtoa nje, hicho ndicho kilichotokea kwa Kibabage,” amesema Mzinga.

Akizungumzia hilo, Daktari wa yanga, Moses Etutu amesema; “Kibabage alipata shida ya Maumivu makali ya kichwa [Migraine] na kushindwa kuendelea na mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Ihefu FC hali iliyopelekea apelekwe hospitali na Joyce Lomalisa kuingia uwanjani kuchukua nafasi yake,” amesema Etutu.

Dokta Etutu, amesema baada ya vipimo mbalimbali walivyomfanyia Kibabage wamejiridhisha kuwa ilikuwa shida ya kawaida na sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.

Yanga ilifanikiwa kushinda mchezo huo dakika ya 101 kwa shuti la Aziz Ki na kuwafanya Wananchi kutinga fainali ambayo watacheza juni 2, 2024 na Azam Fc kule Manyara.

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR YAIKAMUA SIMBA MILIONI 40, KISA MHILU