Home Habari za michezo SABABU ZA JKT KUSHINDWA KUTAMBA ZAWEKWA WAZI

SABABU ZA JKT KUSHINDWA KUTAMBA ZAWEKWA WAZI

JKT TANZANIA WAENDELEZA UONEVU

Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Malale Hamsini amesema sababu kubwa ya timu hiyo kushindwa kutamba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar ni kutokana na wachezaji wa kikosi hicho kupoteza umakini mwishoni.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa juzi Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 huku JKT ikitangulia kupitia kwa Daniel Lyanga kisha Gasper Mwaipasi kusawazisha mwishoni kabisa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Malale alisema walistahili kuondoka na pointi tatu katika mchezo huo ila kitendo cha kukosa umakini na nidhamu kubwa kwenye uzuiaji ndio sababu iliyowafanya kusawazishiwa kirahisi bao hilo.

“Baada ya kupata bao dakika zile za jioni wachezaji waliamini tayari mchezo umeisha hivyo kupoteza umakini kwenye uzuiaji na kuruhusu wapinzani wetu kusawazisha, tunarudi uwanja wa mazoezi kulifanyia kazi,” alisema.

Malale aliongeza licha ya kutowapa furaha mashabiki waliojitokeza kwa wingi kuwapatia sapoti ila amewataka waendelee kuisapoti timu hiyo kwani makosa waliyofanya watayarekebisha kabla ya kucheza na Mashujaa, Oktoba 3.

Mchezo huo ni wa nne kwenye Ligi Kuu Bara kwa JKT msimu huu ambapo ilianza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo kisha ikachapwa mechi mbili mfululizo ikianza na kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Yanga, 2-1 na KMC.

SOMA NA HII  DODOMA FC YAUNGANA NA GWAMBINA FC MSIMU WA 2020/21 ZIPO NDANI YA LIGI KUU BARA