Home Habari za michezo YANGA KILICHOWAPONZA NI DHARAU…MTAPIGWA NYINGI NA RIVERS

YANGA KILICHOWAPONZA NI DHARAU…MTAPIGWA NYINGI NA RIVERS

Kibu Denis | Simba SC

Mechi ya Watani imeamuliwa na saikolojia ya wachezaji, nyuso za wachezaji wa Simba walikuwa na shauku kubwa sana ya kudhihirisha kitu mbele ya wapenzi wa mpira wa miguu ulimwenguni kutokana na kukosolewa kwao kuwa ni kikosi kibovu huku Yanga kwavile wanaongoza ligi na wamepoteza mechi moja tu wakiaminika kuwa ni bora zaidi.

Hali ya kujiamini na kuchukulia mazoea ikaingia kwa mashabiki, wachezaji hadi benchi la ufundi.

Simba walijiandaa sana kiakili kwa hali ya juu hivyo ikawa ni rahisi kwa kuwa ndani ya mchezo katika game plan yao.

Yanga kipindi chote cha kwanza walipoteana kabisa, akili zao zilikuwa hazijatulia, halafu wakawa wana mambo mengi mno uwanjani wakati wachezaji wa Simba walikuwa ni kwenda direct na kwa haraka golini kwa Yanga.

Kutokana na kuwa na utulivu makosa kwa wachezajii wa Simba yakawa ni machache kulinganisha na Yanga waliopotea mchezoni.

Kilichowakuta ni kama surprise, na yote hiyo ni kutokana na kutokuheshimu mpinzani wako.

Kama hii mentality itabadilika, basi kule kwa Rivers Yanga itapigwa goli nyingi sana.

Maana saivi kila mtu anamuonea Simba huruma huku wakijiona wao wapo semi, ila mambo yanaweza kwenda tofauti.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA YANGA...CAF WAISHTUKIA JANJA JANJA YA AL HILAL...WATOA ONYO KALI KWA WASUDANI...