Home Uncategorized IDRISA SULTAN BADO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

IDRISA SULTAN BADO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI


JESHI la Polisi limesema linaendelea kumshikilia Idris Sultan aliyekamatwa Jumanne iliyopita akihusishwa na tuhuma za makosa ya kimtandao likiwemo la kujaribu kuharibu ushahidi.

Mchekeshaji huyo alikamatwa na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar ambako alihojiwa kwa tuhuma za uonevu wa Kimtandao ikiwa ni siku chache baada ya kuweka picha ya zamani ya Rais Magufuli iliyoambatana na video yake akicheka.


Msemaji wa Polisi, David Misime amesema “Tunaendelea kumshikilia kwasababu kubwa mbili; moja ni kuwa baada ya kutakiwa kuripoti Polisi alijaribu kuharibu ushahidi na pili ni katika upelelezi wetu tumebaini makosa mengine ya Kimtandao aliyokuwa akiyafanya.


 “Katika mahojiano tuliyofanya naye tulibaini alitumia namba ya simu isiyo yake katika kutenda uhalifu huo hivyo ushirikiano wake ndio utakaomfanya aendelee kukaa kituoni,”


Lakini pia Wakili wake, Benedict Ishabakaki amesema baada ya mteja wake kuhojiwa walielezwa kuwa dhamana ipo wazi lakini kila wakifuatiliwa wanazungushwa.

SOMA NA HII  YANGA NA MIPANGO YA POINTI TATU ZA AL AHLY