Home Habari za michezo YANGA NA MIPANGO YA POINTI TATU ZA AL AHLY

YANGA NA MIPANGO YA POINTI TATU ZA AL AHLY

Habari za Yanga

Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans umeweka wazi kuwa hesabu katika Ligi ya Mabingwa Afrika ni kupata pointi tatu kwenye kila mchezo ikiwa ni pamoja na Mabingwa watetezi wa Michuano hiyo kutoka Misri, Al Ahly.

Ikumbukwe kwamba Al Ahly waliitoa Simba SC kwenye Michuano ya African Footbal League ‘AFL’ kwa faida ya bao la ugenini baada ya mchezo uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa ubao kusoma Simba SC 2-2 Al Ahly.

Mchezo wa mwisho ulioamua matokeo, Al Ahly 1-1 Simba SC. Hivyo Simba SC waliondolewa kikanuni.

Al Ahly watakutana na Young Africans katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa huku wakinunua kesi hiyo kwa kuweka wazi kuwa wanahitaji pointi tatu.

Afisa Habari wa Young Africans Ally Kamwe ameweka wazi kuwa, mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Al Ahly utakuwa ni muhimu kwao kupata pointi tatu.

“Tutaingia uwanjani kwa nidhamu kwa kuwa tutakabiliana na mabingwa. Hivyo ambacho tutakifanya ni kuwaheshimu na kucheza nao kwa umakini kupata pointi tatu kwa kuwa wapo ambao walishindwa kupata ushindi mbele yao,”

“Katika mashindano haya makubwa kinachoangaliwa ni pointi tatu hilo lipo wazi na wachezaji wanatambua kwamba tuna kazi ngumu ya kufanya kufikia malengo yetu,” amesema Kamwe.

Tayari kikosi cha Young Africans kimeshaelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa Mzunguuko wa kwanza wa Kundi D dhidi ya Chabab Riadhi de Belouizdad ‘CR Belouizdad’ utakaopigwa Ijumaa (Novemba 24).

Kundi D la Ligi ya Mabingwa Barani Afrika lina timu za Young Africans, Chabab Riadhi de Belouizdad ‘CR Belouizdad’ (Algeria), Al Ahly (Misri) na Medeama SC (Ghana).

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA