Home Azam FC WAKATI PRINCE DUBE AKIRUDI ….NADO NNJE MIEZI TISA

WAKATI PRINCE DUBE AKIRUDI ….NADO NNJE MIEZI TISA


WINGA machachari wa Azam Fc, Idd Seleman ‘Nado’ atakuwa nje ya uwanja kwa miezi tisa baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti nchini Afrika Kusini katika hospitali ya Vicent Pallot.

Nado aliondoka nchini jana (Jumanne) alfajiri na kwenda Afrika Kusini kwenda kufanyiwa vipimo kwa mara ya pili kisha alifanyiwa upasuaji.

Kupitia taarifa iliyotolewa na ukurasa wa rasmi wa Instagram  imeeleza ;”Daktari wetu Mwanandi Mwankemwa amethibitisha mshambuliaji wetu Idd Seleman ‘Nado’ atakuwa nje dimba kwa miezi tisa akiuguza majeraha yake ya kukatika mtulinga wa kati wa mguu wake wa kulia.”

Licha ya mchezaji huyo kukosekana katika timu hiyo, mshambuliaji wao mwingine Prince Dube alirejea  uwanjani kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar.

Nado aliumia katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao walishinda 1-0 uliochezwa Novemba 30 katika uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  DILI LA MSUVA SAUDI ARABIA LIKO HIVI....KULIPWA MIL 50 KWA MWEZI....'KUFRU' ZINGINE HIZI HAPA..