Home Habari za michezo DILI LA MSUVA SAUDI ARABIA LIKO HIVI….KULIPWA MIL 50 KWA MWEZI….’KUFRU’ ZINGINE...

DILI LA MSUVA SAUDI ARABIA LIKO HIVI….KULIPWA MIL 50 KWA MWEZI….’KUFRU’ ZINGINE HIZI HAPA..

Habari za Michezo leo

Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Tanzania, Simon Msuva ndio basi tena Yanga. Hii ni baada ya kutambulishwa Al Najmah inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Saudi Arabia.

Kipindi cha dirisha dogo la usajili kulikuwa na tetesi za nyota huyo aliyewahi kutamba akiwa na Yanga, huenda akarejea kwenye timu hiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara akiwa mchezaji huru baada ya kuvunjiwa mkataba na JS Kabylie ya Algeria.

Wakati wengi wakiamini anarudi Jangwani alikioondoka tangu msimu wa 2017/18 na kutua Difaa El Jadida, msuva hakurejea kucheza Ligi Kuu Bara na ameendelea kucheza nje ya nchi ikiwa ni mara ya pili anarudi Saudi Arabia kucheza Ligi Daraja la Kwanza.

Baada ya utambulisho huo, kwenye akaunti ya klabu ya Instagram, Msuva aliongea akifurahia kujiunga na timu hiyo ambayo kwenye msimamo wa ligi hiyo, iko nafasi ya tisa baada ya kucheza michezo 18 na ina pointi 25.

“Nafurahia kusaini Al Najma, nafurahi kurudi Saudi Arabia na tutaonana baadaye,” alisema Msuva.

Msuva atajiunga na timu hiyo baada ya kumaliza mechi za Stars ambayo inacheza leo na DR Congo mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kwenye Fainali za Afcon zinazoendelea Ivory Coast.

Hii ni timu ya tano kwake kucheza nje ya nchi tangu alivyoondoka Yanga msimu wa 2017-18 na amepita Difaa El Jadida na Wydad Casablanca za Morocco, Al Qadsiah ya Saudi Arabia na JS Kabylie ya Algeria.

Kwenye Fainali za Afcon ameifungia bao moja Stars dhjidi ya Zambia na kufikisha mabao 22 tangu aanze kuichezea timu hiyo.

MSUVA MWENYEWE HUYU HAPA..

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa Ivory Coast, Msuva amesema ni kweli amemalizana na timu hiyo kwa mkataba wa muda huo.

“Nakwenda kucheza nchi ambayo tayari nina uzoefu nayo, sioni shida yotote itakayonisumbua. Kilichobadilika ni timu tu, natumaini nitafanya kile kitakachonipeleka kwa usahihi,” amsema mshambuliaji huyo mwenye bao moja katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) zinazoendelea nchini humo.

“Kuhusina na kusaini mkataba kwa muda mfupi hiyo ni mipango ambayo ipo sasa. Kitakachofuata tumuachie Mungu, sasa tuzungumze dili lililokamilika.”

Msuva amesema anafurahi kupata timu katika muda wa dirisha na anafurahia hilo, lakini mambo mengi yalikuwa yanazungumza sasa ni muda wake wa kufanya kazi mara baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa.

Kutua kwake Alnajmah FC atakuwa ametimiza timu tano nje ya nchi tangu alipoondoka Yanga msimu wa 2017-18 akipita katika timu za Difaa El Jadida na Wydad Casablanca za Morocco, Al Qadsiah ya Saudia Arabia na JS Kabylie ya Algeria.

Hata hivyo inafahamika kuwa Msuva amesaini mkataba wa Mwaka mmoja , huku chanzo chetu cha karibu kutoka huku kikisema kuwa atakuwa akilipwa mshahahwa wa Dola 20,000 kwa mwezi sawa a zaidi ya Milioni 50 za kitanzania.

SOMA NA HII  BENCHIKHA AWAPIGA MKWARA MASTAA WANAOCHEZA 'KIFAZA FAZA' SIMBA...