Home Uncategorized MKE AMTWANGIA SIMU MCHEZAJI AKIWA UWANJANI

MKE AMTWANGIA SIMU MCHEZAJI AKIWA UWANJANI


PETER Crouch nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya England amesema kuwa mkewe alikuwa hapendi kuskia kitu kinaitwa mpira wa miguu. 

Nyota huyo aliyekipiga pia ndani ya Klabu za Liverpool na Stoke City ambaye sifa yake kubwa ilikuwa ni urefu na mbaya kumalizia mipira ya juu anasema kuwa aliwahi kupigiwa simu na mkewe kabla ya mechi kuanza.

Abbey Clancy ambaye ndiye ubavu wake alimtwangia simu akiwa uwanjani na kumuuliza yupo wapi. 

“Mke wangu hapendi kitu kinaitwa mpira wa miguu. Siku moja alinipigia simu dakika 10 kabla ya mpira kuanza na kuniuliza nipo wapi?”

SOMA NA HII  KUMEKUCHA SIMBA, MBELIGJI APEWA MECHI TATU AKIZINGUA MOJA KUPIGWA CHINI JUMLAJUMLA