Home Uncategorized BUNDESLIGA YAREJEA KWA KISHINDO, HAALAD AANZA YAKE

BUNDESLIGA YAREJEA KWA KISHINDO, HAALAD AANZA YAKE


LIGI Kuu ya nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga imerejea jana rasmi ambapo kazi ilianza kwa mechi sita kupigwa kwenye viwanja tofauti huku mamilioni ya mashabiki wakiifuatilia Ligi hiyo.

Ligi hiyo ilisimama tangu Machi mwaka huu kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona ambavyo vinaivurugavuruga dunia na mechi zinachezwa bila uwepo wa mashabiki kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.


Mechi ambayo ilikuwa na hisia na ilifuatiliwa na wengi ni pamoja na ile iliyowakutanisha Borussia Dortmund ambao walishinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Schalke.

Mabao ya Dortmund yalifungwa na Erling Braut Haalad dk 29, Raphael Guerreiro dk 45 na 63 pamoja na Thorgan Hazard dk 48.

Matokeo hayo yanaifanya Dortmund ijikusanyie jumla ya pointi 54 kibindoni ikiwa nafasi ya pili huku Schalke ikiwa na pointi 37 nafasi ya nane zote zimecheza mechi 26.

SOMA NA HII  MAMBO NI MAGUMU SASA NDANI YA SIMBA, MBELIGIJI ATOA LA MOYONI