Home Uncategorized MAPROO WANNE, MITAMBO YA MABAO NDANI YA YANGA PANGA LINAWAHUSU

MAPROO WANNE, MITAMBO YA MABAO NDANI YA YANGA PANGA LINAWAHUSU

INAELEZWA kuwa nyota wanne wa Klabu ya Yanga panga linawahusu msimu ujao kutokana na kushindwa kufiti ndani ya kikosi cha kwanza.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu Luc Eymael ikiwa imecheza mechi 27 ipo nafasi ya tatu na kibindoni ina pointi zake 51 ipo kwenye mpango wa kuboresha kikosi chao msimu ujao.

Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa wageni ambao hawapo kwenye hesabu za Eymael ni pamoja  na David Molinga raia wa Congo, Patrick Sibomana raia wa Rwanda.

Wengine ni Erick Kabamba raia wa Zambia pamoja na Yikpe Gnamien raia wa Ivory Coast mwili jumba.

Nyota hao wamehusika Kwenye mabao 17 kati ya 31 yaliyofungwa na Yanga, ambapo Molinga amefunga nane, Sibomana amefunga matano na pasi tatu za mabao huku Yikpe akifunga bao moja. 

SOMA NA HII  MBEYA CITY V SIMBA NGOMA NZITO LEO SOKOINE