Home Simba SC SIMBA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO, YAIPIGA DODOMA JIJI 3-0

SIMBA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO, YAIPIGA DODOMA JIJI 3-0

 MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho,  Simba, leo Mei 26 wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Kombe la Shirikisho,  hatua ya robo fainali. 

John Bocco alipachika mabao mawili dakika ya 22 na 41 na kuwafanya Simba kwenda mapumziko ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 2-0 Dodoma Jiji.

Kipindi cha pili, Dodoma Jiji waliongeza jitihada kusaka bao la ushindi ila walikwama kupenya ngome ya Pascal Wawa na Kened Juma ambao walikuwa wakicheza kwa maelewano.

Bao la tatu lilipachikwa na Meddie Kagere ambaye anafikisha jumla ya mabao matatu ndani ya Kombe la Shirikisho. 

Ushindi huo unaifanya Simba kutinga hatua ya nusu fainali na itakutana na Azam FC ambayo imeshinda leo mabao 3-1 dhidi ya Rhino Rangers.

SOMA NA HII  MKUTANO MKUU SIMBA:..JINA LA MANARA LATAJWA MEZA KUU...WANACHAMA WASHANGILIA...