Home Ligi Kuu KMC YAIVUTIA KASI NAMUNGO FC

KMC YAIVUTIA KASI NAMUNGO FC


KLABU ya KMC FC imeanza kufanya maandalizi kuelekea katika mchezo wake dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kuchezwa Februari 4, Uwanja wa Uhuru.

Mchezo huo utachezwa majira ya saa 10:00 jioni ikiwa ni wa kiporo kutokana na Namungo FC kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania iliyotolewa Januari 30.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kikosi kinaendelea mazoezi chini chini ya Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo.

 “Maandalizi yapo vizuri na mpango mkubwa ni kupata pointi tatu muhimu ndani ya uwanja kwa kuwa tunahitaji kuendelea kujiweka sawa.

“Kila mchezaji amekuwa na morali kubwa kuelekea kwenye mchezo huo na mechi za kirafiki ambazo tumekuwa tukicheza ni mwendelezo wa kukiweka kikosi sawa,” .

KMC ipo nafasi ya 7 kwenye msimamo baada ya kucheza jumla ya mechi 17 kibindoni ina pointi 22.

Inakutana na Namungo FC ambayo ipo nafasi ya 15 na pointi zake kibindoni ni 18 baada ya kucheza mechi 14.


SOMA NA HII  ULE MPAPATUKO WA LIGI KUU YA NBC..KUENDELEA TENA LEO...WAKUBWA WOTE 'MACHO KODO' KWENYE VIWANJA WIWILI....