Home Habari za michezo ILI KUKABILIANA NA KUNDI D GAMONDI AITUMIA LIGI KUU

ILI KUKABILIANA NA KUNDI D GAMONDI AITUMIA LIGI KUU

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Miguel Angel Gamondi, ameanza mchakato kuwapeleleza wapinzania waliopangwa moja katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imepangwa Kundi D na timu za Al Ahly (Misri), Medeama (Ghana) CR Belouizdad (Algeria).

Mechi za Gamondi ameamua kufanya upelelezi huo kujua ubora na udhaifu wa wapinzani wake, lengo ni kumrahisishia kupata mazuri atakapokutana nao.

Mechi za kwanza za hatua ya makundi ya michuano hiyo zinatarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 24 na 25 mwaka huu, huku Young Africans ikianzia ugenini dhidi ya CR Belouizdad (Algeria).

Akizungumza jijini Dar es salaam, Kocha huyo amesema ameanza mchakato wa kuzifuatilia timu hizo kujua mbinu wanazotumia, imrahisishie kazi.

Muargentina huyo amesema, lengo lake ni kuiongoza timu yake iwe kinara katika Kundi hilo lililosheheni timu zenye ushindani.

“Nitahakikisha nawafuatilia wapinzani wangu kujua ni mbinu gani wanazozitumia na kutusaidia sisi kuweza kushinda katika kila mchezo na kuongoza Kundi letu na kutinga Robo Fainali” amesema.

Kocha huyo amesema atatumia michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kukifua kikosi chake kuwa bora dhidi ya wapinzani wake katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Young Africans ilitinga hatua Makundi baada ya kufanya vyema katika hatua ya kwanza na ya pili ya mtoano wa michuano hiyo.

Wananchi walianza michuano hiyo kwa kuitoa Asas ya Djibouti kwa mabao 7-1, kabla ya kuifunga Al Merrikh ya Sudan mabao 3-0.

SOMA NA HII  MORRISON AWAKIMBIZA MAKOMANDOO YANGA USIKU, BALAA LA SIMBA ACHA,NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO