Home Habari za michezo BARBARA AZIDI KUKINUKISHA HUKO….ATUPA DONGO JIPYA KWA MO DEWJI….

BARBARA AZIDI KUKINUKISHA HUKO….ATUPA DONGO JIPYA KWA MO DEWJI….

Habari za Michezo

Barbara Gonzalez ameendelea kutoa kauli zake ambazo haijulikani anamlenga nani kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Hii leo, Barbara amekuja na hii mpya:

“Binaadamu tuna tatizo la kusahau. Hakuna mwenye cheo cha milele! Ubabe utafikia kikomo chake. Kiburi ni cha muda tu. Dharau zina mwisho wake. Kuwa mpole Kaka. Power and influence is temporary!”

Kabla ya hiyo, Barbara amewahi kutoa kauli kadhaa ambapo moja wapo ilichukuliwa na mchezaji wa Simba SC, Clotus Chama na watu kujaribu kuihusanisha na masuala yake ya kimkataba ambayo hata hivyo yalitangazwa kuisha na Chama anatarajia kujiunga na wenzake kambini Uturuki.

“Usilipize ubaya kwa ubaya, lakini usiwe mnyonge kudai haki zako!” hii ndiyo aliyoichukua Chama.

SOMA NA HII  HAWA HAPA MAKOCHA WANOSUKUMA NDINGA ZA MAANA LIGI KUU...