Home Habari za michezo TETESI: HII HAPA MASHINE YA KAZI INAYOTAJWA KUTUA SIMBA….JAMAA NI BALAA NA...

TETESI: HII HAPA MASHINE YA KAZI INAYOTAJWA KUTUA SIMBA….JAMAA NI BALAA NA NUSU…

Tetesi za Usajili Simba

Kocha Mkuu wa FC Nouadhibou, Aritz López Garai ameweka wazi kuwa kiungo wa timu hiyo Mohsine Bodda anajiandaa kuondoka ndani ya kikosi hicho mwishoni mwa msimu huu.

Simba SC wamekuwa wakitajwa kuiwinda saini nyota huyo raia wa Mauritania aliyelisaidia taifa hilo kufanya vyema kwenye michuano ya AFCON mwanzoni mwa mwaka huu.

Pia, klabu kadhaa za nchini Morocco zikiongozwa na Wydad Casablanca zinaiwinda saini ya kiungo huyo.

Mchambuzi wa michezo kwenye kituo cha Azam TV , Godlisten Muro amedai kuwa endapo Simba itamnasa kiungo huyo itakuwa imelamba dume kwani kazi aliyoifanya kwenye michuano ya AFCON mwaka huu imemfanya kuwa mchezaji anayetakiwa na klabu kubw zote Afrika.

Aidha katika hatua nyingine, Tetesi za usajili zinaeleza kuwa, Klabu ya Simba iko katika mazungumzo na golikipa wa Tabora United, John Noble ili kuchukua nafasi ya kipa wao anayetajwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Ayoub Lakred amekuwa kwenye kiwango bora sana kwa sasa huku akiwabeba wekundu hao wa msimbazi lakini ameshitua Kwa kuwaambia kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu huu mkataba wake utakapomalizika.

Taarifa zinaeleza kwamba, Simba wanamuona Noble kuwa kipa sahihi wa kuidakia timu hiyo kwani ni golikipa mwenye uwezo wa juu akiwahi kuichezea klabu ya Enyimba na timu ya Taifa ya Nigeria.

Kabla ya kumsajili Lakred, klabu ya Simba ilikuwa ikimuwinda kipa huyo kabla ya kuzidiwa kete na Tabora United. Hata alipotua nchini, Simba walijaribu kumsajili ili kuipiku Tabora jambo ambalo liliwazindua viongozi wa Tabora na kumsainisha mkataba haraka.

John Noble alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Tabora United hivyo haitakuwa shida Kwa Simba kumpata na pia mchezaji huyo hawezi kukataa fursa ya kuitumikia klabu hiyo inayoshiriki michuano ya vilabu barani Afrika mara kwa mara.

SOMA NA HII  MASHABIKI CONGO WATUMA VIDEO KWA ENG HESRI NA YANGA KUTAKA MSAADA...ISHU IKO HIVI...