Home Habari za michezo MASHABIKI CONGO WATUMA VIDEO KWA ENG HESRI NA YANGA KUTAKA MSAADA…ISHU IKO...

MASHABIKI CONGO WATUMA VIDEO KWA ENG HESRI NA YANGA KUTAKA MSAADA…ISHU IKO HIVI…

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said

Hapo awali nchini DR Congo kulikuwa na kijiji kinaitwa Ngoma, lakini mpelelezi Gustav Adolf von Götzen alishindwa kutamka jina la Ngoma akatamka Goma ndipo mji huo ukaanza kutambulika hivo.

Mji wa Goma ni moja ya miji maarufu sana nchini DR Congo. Ni mji ambao umepitia changamoto mbalimbali, kama vile vita, maafa na milipuko ya Volkano.

Mashirika mbalimbali ya kimataifa yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kusaidia wahanga mbalimbali katika mji huu lakini bado umasikini umeendeleza kuusakama mji huu.

Tunafahamu kumekuwa na machafuko mara kwa mara na wenyeji wa mji huu wamekuwa wahitaji wakubwa katika masuala ya kiusalama.

Kuna video inaonekana baadhi ya wenyeji wa mji wa Goma wakiomba msaada, zamu hii sio msaada wa kiusalama, la hasha ni msaada wa upendo.

Mwanamama mmoja kutoka Rushturu Goma, amesikika kwenye video iliyosambaa mitandaoni akiomba msaada wa hali na mali kutoka kwa Rais wa Yanga SC Injinia Hersi Said.

Inaonekana wenyeji mji wa Goma ambao upo karibu ni mkoa wa Kigoma, wana shida kubwa ya upendo. Upendo ambao umesambazwa na klabu ya Yanga hivi karibuni kuwafikia wenye uhitaji.

Kwa muda sasa klabu ya Yanga imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa wahitaji. Kimsingi mfumo huu umeweka alama kwenye mioyo ya watanzania walio wengi.

Upendo huo umesambaa hadi nchi jirani ambao tunaona wananchi wa DR Congo wakitamani uongozi wa klabu ya Yanga kwenda kuwashika mkono na kuwafariji kutokana na changamoto wanazokutana nazo.

Haya ni matunda ya kampeni hii ya Yanga kurudisha kwa jamii na kuwafariji kwa chochote wahitaji mbalimbali.

Rais wa Yanga SC ameguswa sana na video hiyo;

“Baada ya kuona video hiyo, imenigusa sana, nimejiuliza sana ni jambo lipi hili kubwa ambalo tumefanya kiasi cha ndugu zetu kuona umuhimu wetu kwao? Moyo wangu umeniambia hakuna kubwa zaidi ya upendo ambao klabu imekuwa ikionesha kwa wahitaji. Kumbe kutembelea wahitaji kumegusa sehemu kubwa sana ya maisha ya walio wengi.”

“Inawezekana hatukuweza kutimiza haja ya maisha yao lakini kwa kiasi fulani tulipeleka faraja ambayo imeweka alama kwa tuliowafikia na wale ambao bado. Mimi na uongozi wa Yanga tumebeba maombi ya ndugu zetu wa Goma kwa uzito wa kipekee na tunatamani sana siku moja kufurahi nao pamoja.”

Kwa ujumbe huu Rais wa Yanga akishirikiana na watendaji mbalimbali wa Yanga SC watafanya kila jitihada kuwafariji na kuwaonesha upendo ndugu zetu hawa DR Congo wanaokumbana na adha mbalimbali za kimaisha.

Uongozi wa klabu umelipokea ombi la ndugu hawa wa Goma na klabu ipo kwenye mchakato wa kuratibu namna ambavyo itaweza kuwafariji ndugu zetu.

Hii ndio dira ya klabu ya wananchi, kuhakikisha kuwa wapo karibu na wananchi na kuwajali wananchi kwa kila.

SOMA NA HII  MAXI NZEGELI YAMKUTA YA MAYELE YANGA