Home Habari za michezo MBOWE: SIWATAKII SIMBA MAMBO MEMA……JEZI ZA YANGA HATA ZIWEJE SIVAI NG’OO….

MBOWE: SIWATAKII SIMBA MAMBO MEMA……JEZI ZA YANGA HATA ZIWEJE SIVAI NG’OO….

Mbowe na Simba

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema anaishabikia Klabu ya Yanga (Wananchi) lakini hawezi kuvaa jezi zao kwani zina rangi (kijani na njano) ambazo ni rangi za wapinzani wake kisiasa (Chama Cha Mapinduzi – CCM).

Mbowe amesema hayo hivi karibuni wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa na kitaifa kwa ujumla kufuatia vyama vya siasa kuruhusiwa na Rais Samia Suluhu kufanya mikutano ya hadhara iliyokuwa imepigwa marufuku kwa miaka kadhaa.

“Timu yangu ni Wananchi, na mimi ni Mwananchi kiasili, lakini nakwazika sana ninaposhindwa kuvaa jezi ya timu yangu. Niliwahi kuwa mmoja wa wadhamini wa Yanga, naipenda sana, hata wakati ule tuliwapa jezi za Club Bilcanas ilikuwa ni nyeusi na nyeupe, hazikuwa njano na kijani. Wakati ule hata vuguvugu la kisiasa halikuwepo sana kiasi hicho.

“Michezo ni furaha, inaunganisha watu, ukitazama namna ambavyo michezo inaunganisha watu unatamani Serikali ingeona ulazima wa kuwekeza kwenye michezo vya kutosha ili kuleta watu pamoja, lakini ukitazama sasa hivi unaona uwekezaji wa Serikali ni duni.

“Kwa Tanzania naiunga mkono Yanga, lakini Simba nawapenda siwachukii japo siwatakii mema sana, ila nawapenda kama Watanzania wenzangu, sina nongwa nao. Nje naisapoti Real Madrid (ya Hispania) na Liverpool (ya Uingereza) japo kwa sasa tunapitia wakati mgumu sana.

“Michezo sio tu furaha kwa taifa, michezo ni uchumi, ni biashara. Unapoona nchi ndogo kama Qatar wanatumia mabilioni ya dola kuwekeza kwa ajili ya kuandaa kombe la Dunia ujue hiyo ni pesa. Mpira Duniani ni tasnia kubwa.

“Kwa Tanzania, Simba wamefanya vizuri Kimataifa kwa miaka ya hivi karibuni, sio tu kwa ustawi wa Taifa lakini hii inasaidia kutangaza nchi, exposure kwa wachezaji wetu na kujiuza kimataifa. Kwenye mpira ukiwekeza lazima upate faida kubwa. Sisi kama Taifa tunatakiwa kuweka nguvu kubwa na pesa ya kutosha kuwekeza katika biashara,” amesema Mbowe.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA MAMBO MAGUMU KWA WAARABU...ADEBAYOR AANZA KUJISOGEZA SIMBA KIAINA...

1 COMMENT

  1. Great article! We will bee linking to this great rticle on our site.
    Keeep up thee good writing.

    Visit mmy web-site: Caliente (Robin)