Home Habari za michezo BAADA YA KUONA MAMBO MAGUMU KWA WAARABU…ADEBAYOR AANZA KUJISOGEZA SIMBA KIAINA…

BAADA YA KUONA MAMBO MAGUMU KWA WAARABU…ADEBAYOR AANZA KUJISOGEZA SIMBA KIAINA…

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Niger na Klabu ya RS Berkane ya Morocco Victorien Adebayor amesema anatarajia siku moja atacheza Simba SC, kufuatia kuvutiwa na utamaduni wa Klabu hiyo ya Msimbazi, Dar es salaam.

Adebayo alikaribia kutua Simba SC wakati wa Usajili wa Mwanzoni mwa msimu huu, lakini RS Berkane iliizidi kete Klabu hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kumwaga fedha nyingi za usajili, wakimtoa USGN ya Niger.

Akizungumza kutoka nchini Morocco Adebayor amesema, bado anatamani kucheza Simba SC katika maisha yake, kwa sababu anajua klabu hiyo ina mambo mengi ambayo anaendana nayo, hususan mapenzi alioonyeshwa na Mashabiki alipotua Dar es salaam kwa mchezo wa Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu uliopita.

“Nilitamani kucheza Simba SC, ni Klabu ambayo ilionyesha kila hatua ya kunihitaji, hasa mashabiki wao nawakumbuka sana upendo walionionesha nikiwa hapo Tanzania”

“Wakati ule kulikuwa na ugumu kwa Simba SC walitakiwa kukamilisha dili lile huku wakishindana na Klabu nyingine iliyohitaji huduma yangu, kwa hiyo ilikua ngumu sana.”

“Bado ninaikumbuka Simba SC nawakumbuka sana Mashabiki wake, naamini utakuja wakati ninaweza kuja kuichezea Simba SC hivi karibuni.” amesema Adebayor

Tangu alipojiunga na RS Berkane mwanzoni mwa msimu huu, Adebayor amekua na wakati mgumu wa kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo, kama ilivyokua USGN ambapo alitegemewa sana katika safu ya ushambuliaji.

SOMA NA HII  AZAM FC KUITIBULIA SIMBA DILI LA KUMNASA MAKABI...MABOSI CHAMAZI WATENGA DAU NONO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here