Home Habari za michezo KOCHA MAARUFU AFRIKA AIPELEKA YANGA SC NUSU FAINAL CAF…AWAPA MBINU ZA KUPITA…

KOCHA MAARUFU AFRIKA AIPELEKA YANGA SC NUSU FAINAL CAF…AWAPA MBINU ZA KUPITA…

Habari za Yanga

Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameipa nafasi kubwa klabu hiyo kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kwa kuichapa Rivewrs United ya Nigeria.

Yanga SC itaanzia ugenini Nigeria kucheza mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa hatua hiyo April 23, kabla ya kumalizia nyumbani jijini Dar es salaam katika Uwanja  wa Benjamin Mkapa April 30.

Kocha Micho ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Uganda The Cranes, amesema kwa uzoefu alionao kwa timu za Afrika anaiona Yanga SC kuwa na nafasi kubwa na uwezekanao wa kufuzu kwenda nusu fainali kwa asilimia 75 kutokana na mabadiliko makubwa iliyoyafanya kikosini.

Kocha huyo aliyeinoa Yanga SC mwaka 2007, amesema kitendo cha Klabu hiyo kuwa na Mshambuliaji Fiston Mayele aliye kinara wa mabao Ligi Kuu akiwa na 16 na mwenye mwendelezo mzuri wa kufunga, anaamini kitaendelea kuibeba timu hiyo sambamba na nyota wengine ambao wameipigania timu hiyo tangu ilipokuwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Nimeifundisha Yanga. Kuna mabadiliko makubwa ya kiuchezaji na hata aina ya wachezaji. Niseme mechi na Rivers inatabirika kwani sasa hivi Young Africans ina kiungo mzuri kama Khalid Aucho ambaye anaichezea timu ya taifa ya Uganda, Mayele na wengine wanaoweza kuipigania na kuivusha,” amesema.

Mshindi wa Jumla kati ya Young Africans na Rivers United atakutana na mshindi wa Jumla wa mchezo kati ya Pyramids ya Misri na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

SOMA NA HII  DAKIKA KADHAA KABLA YA KUKIPIGA NA ALGERIA...SAMATTA AIBUKA NA KAULI HII YA KIBABE KWA MASHABIKI...