Home Habari za michezo KISA KUMTANDIKA SANE NGUMI ZA USO…MANE APIGWA FAINI YA MIL 724….HUENDA AKAPIGWA...

KISA KUMTANDIKA SANE NGUMI ZA USO…MANE APIGWA FAINI YA MIL 724….HUENDA AKAPIGWA BEI MAZIMA…

Sadio Mane

Baada ya Sadio Mane kumpiga mchezaji mwenzake wa bayern Munich, Leroy Sane wiki iliyopita nyota huyo amepigwa faini ya pauni 250,000, (Sh.724,445,000).

Pia inatajwa kuwa staa huyo raia wa Senegal yupo kwenye hesabu za kuuzwa mwishoni mwa msimu huu.

Mane alimchapa ngumi ya mdomo Sane kwenye chumba cha kubadilishia nguo wiki iliyopita kwa madai kuwa Sane alimkejeli kwa lugha na vitendo vya kibaguzi baada ya mchezo dhidi ya Manchester City.

Sane alionekana akiwa amevimba mdomo wakati Bayern Munich walipoivaa Hoffenheim wikiendi iliyopita na Mane hakuwepo kwenye mchezo huo wa Bundesliga.

Mane amesimamishwa kwa kitendo hicho huku akikatwa mshahara wake wa pauni milioni 17, (sh.49.2) kwa mwaka. Hii ni faini kubwa kwa Bayern Munich kutolewa katika historia yao.

SOMA NA HII  SIMBA SIO KINYONGE ATUA BOTSWANA KIFALME