Home Simba SC KUMBE KAIZER CHIEF WALIMTAKA LUIS KWA PESA NYINGI ZAIDI YA DAU LA...

KUMBE KAIZER CHIEF WALIMTAKA LUIS KWA PESA NYINGI ZAIDI YA DAU LA AL AHLY


KAIZER Chiefs waliongeza dau kwa mzigo Simba, ili kumpata  Luis Miqussone aliyeko kwenye hatua za mwisho kutimkia Al Ahly.

Habari za uhakika ambazo gazeti la Mwanaspoti imezipata ndani ya Simba ni kwamba, Kaizer Chiefs walionyesha nia ya kuweka mezani Sh 1.5 Bil ikiwa imezidi ile Bil 1 ya Al Ahly ya Misri.

Lakini gazeti la Mwanaspoti linajua kwamba Luis amewaambia marafiki zake wa karibu ndani ya Simba kwamba anakwenda Al Ahly.

Hadi jana Uongozi wa Ahly ulikamilisha rasmi uhamisho wa winga huyo kutoka Simba kwa ada ya Dola 900,000

Usajili wa winga huyo umekamilika  baada ya kufikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo

Mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Afrika mara 10 walifikia makubaliano na Simba tangu wiki iliyopita na kilichobakia ilikuwa ni kumalizana na mchezaji huyo.

SOMA NA HII  IMEFICHUKAAH...HII HAPA SABABU YA MO DEWJI 'KUKACHA' MSIBA WA HANS POPE