Home Habari za michezo AHMED ALLY:- KAGERA SUGAR WAMEKUJA WAKATI M’BAYA SANA …

AHMED ALLY:- KAGERA SUGAR WAMEKUJA WAKATI M’BAYA SANA …

Habari za Simba leo

Wakati Simba wakijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugara katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Simba hawana jambo jingine katika mchezo huo zaidi ya kuondoka na alama tatu.

Akizungumza katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari, Ahmed Ally anasema;

“Maandalizi ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar yanakwenda vizuri na nyie wote mnaona tulivyoimarika. Wamekuja wakati mbaya. Tunakwenda uwanjani tukiwa na uhakika asilimia 100. Kesho saa 10:00 tunakwenda kuchukua alama tatu. Lakini pia itakuwa mechi ya kwanza kwa mtaalamu kocha Abdelhak Benchikha.”- Ahmed Ally.

“Mechi ya Kagera Sugar ni maandalizi ya mechi dhidi ya Wydad na tiketi zake zitaanza kuuzwa kesho. Mechi dhidi ya Wydad itakuwa tarehe 19 Desemba, 2023 saa 10:00 jioni na tutaingia tukiwa na option moja tu, kushinda. Tutaweka rehani roho zetu ili kushinda.”- Ahmed Ally.

SOMA NA HII  ZILIZOPO....YANGA WAONGEZA MKONGO MWINGINE KIKOSINI...NI BEKI LA KAZI HASWA...ACHOTEWA MAMILION YA KUSAINI...