Home Habari za michezo SIMBA KUMTUMIA MISO MISONDO KUWAMALIZA WYDAD KWENYE LIGI YA MABINGWA AFRIKA..

SIMBA KUMTUMIA MISO MISONDO KUWAMALIZA WYDAD KWENYE LIGI YA MABINGWA AFRIKA..

Habari za Simba

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema maandalizi ya mechi mbili zilizopo mbele yao ya hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco na Jwaneng Gallaxy ya Botswana inaendelea vizuri.

“Tiketi ya mchezo dhidi ya Wydad Casablanca zimeanza kuuzwa leo, shabiki anayekuja kwenye mechi yetu ya Mtibwa Sugar basi shabiki amalizanae kabisa na suala la kununua tiketi ya Desemba 19, ya kutafuta pointi tatu muhimu ili kwenda hatua ya robo fainali.

Mchezo wetu na Wydad tutacheza saa 10 : 00 alasiri, katika michezo hii miwili tumeweka rehani roho zetu jambo moja tu ambali tunalihitaji ni ushindi tu siku hiyo,” alisema Ahmed.

Alieleza kuwa ni mechi ngumu na wanafahamu ubora wa Wydad Casablanca lazima mashabiki wajitikeze kwa wingi kusapoti timu uwanjani ambao wamedhamilia kupambana kwa jasho ili kusaka ushindi wa idadi kubwa ya mabao mengi.

“Viingilio mzunguko ni Shilling 5,000 hawa ndugu zangu wana viti vingi basi yale mafuriko ya halaiki ya Wydad Casablanca basi wajjitokeze kwa wingi kununua tiketi, VIP C 10,000, B, 20,000, VIP A 30,000 na 150,000 platinum.

Tushikamane kwa pamoja na kujitokeza uwanjani kwa sababu ya kufanikiwa kwenye malengo yetu ya kuhakikisha tunaenda kutafuta alama sita ambazo tufikie malengo yetu ni nusu fainali,” alisema Ahmed.

Kuhusu wapinzani wao Wydad Casablanca, alisema bado hawajatoa taarifa ya lini watawasili lakini waamuzi wanatoka sehemu mbalimbali, akiwemo pirato wa mchezo huo anatoka Gabon, Pierre Ghislain, akisaidiwa na Boris Marlaise (Gabon) na Carine Atezambong (Cameron)

Aliongeza kuwa Mgeni rasmi wa mchezo huo ni Kocha wao, Benchikha kwa kuwa ni kocha bora namba tatu kwa Afrika na pia ameifanya Simba kuwa na mabadiliko makubwa.

Meneja huyo Alisisitiza kuwa licha ya kuwa na alama mbili kwenye kundi lao lakini wanaimani ya Simba inafanikiwa kutinga robo fainali kwa kushinda mchezo huo wa jumanne na kila Mwanasimba anatakiwa kuiunga mkono timu ya kwenda hatua hiyo.

“Hii siku ya Jumanne kwetu Jamhuri ya watu wa Simba tunaifanya nusu siku (Mnyama Tuesday half Day) kwa sababu tunahitaji mashabiki wa Simba kuja kwa wingi uwanjani, tunakuja na kauli ya haijakwisha hadi ifikie mwisho,” alisema Ahmed.

Aliongeza kuwa safari hii wametoa kazi kwa wenyeviti wa matawi kuhamasisha wanachama wao kujitokeza uwanjani na matawi 50 ya mwanzo watapewa kibali maalum cha gari kuingia uwanjani.

Ahmed alisema Desemba 16, watakuwa na hamasa kubwa ambalo litakuwa Mbagara na kutakuwa na burudani na DJ Miso Misondo anatarajia kuwepo kwenye hamasa hizo.

Kwa upande wa DJ Miso Misondo alisema anafurahi kuwa sehemu ya Simba na kupewa fursa ya kuwa sehemu ya kutoa burudani na kutengeneza ngoma kali inayowahusu Simba.

“Kuna kitu maalum ambayo tumeaanda kwa ajili ya mashabiki wa Simba (tumewaandalia Dimbe) kubwa, lakini naomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika hamasa siku ya jumamosi,” alisema Dj Miso Misondo

SOMA NA HII  GOMES ANAAMINI WAFUNGAJI WAKE WATAMALIZA NAFASI YA KWANZA KWA UTUPIAJI