Home Habari za michezo BAADA YA KUSAIDI DILI JIPYA YANGA SC…JOB AFUNGUKA A-Z SABABU ZA KUITOSA...

BAADA YA KUSAIDI DILI JIPYA YANGA SC…JOB AFUNGUKA A-Z SABABU ZA KUITOSA SIMBA SC…

Habari za Yanga SC

Beki wa Kati wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga SC, Dickson Job amesema ilikua lazima aendelee kubaki klabuni hapo, na ndio maana amekubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuhudumu kwenye klabu hiyo.

Job alikuwa anahusishwa na kujiunga Simba SC mwishoni mwa msimu huu, huku ikitajwa pia kuwa na dili zingine nje ya nchi, lakini Uongozi wa Young Africans mwishoni mwa juma lililopita ulitoa picha za mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka miwili.

Dickson amesema ilikuwa lazima kwake kubaki Young Africans kwani ni timu ambayo amekuwa nayo kwenye wakati mzuri, pia imempa kile ambacho amekihitaji.

“Kikubwa ni kuwashukuru viongozi na mashabiki wote wa Young Africans kwa kuniamini na kuamua kuniongezea mkataba, nami kama mchezaji na nitaendelea kuipambania nembo kila ninapopata nafasi,” amesema Job aliyesajiliwa na Yanga wakati wa Dirisha Dogo misimu miwili iliyopita akitokea Mtibwa Sugar.

Tangu aliposajiliwa Yanga SC, Beki huyo wa kati amekuwa katika kiwango kizuri ndani ya miaka miwili huku akiwa sehemu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na huku akibadilishana nafasi na nyota wengine wa nafasi hiyo kikosini akiwamo nahodha Bakar Mwamnyeto, Yannick Bangala, Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ pamoja, huku Shaibu Abdallah ‘Ninja’ na Mamadou Doumbia wakikosa nafasi kikosi cha kwanza.

Job mwenye bao moja katika Ligi Kuu Bara alikuwa kwenye sehemu ya wachezaji wa timu ya taifa ambayo inacheza michuano ya Kombe la Mataifa kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) na kwenye michezo ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI vs AL AHLY...SIMBA WAMTUPIA 'MSALA' WOTE BENCHIKHA....