Home Habari za michezo YANGA YAIPITA SIMBA KWENYE KLABU ZENYE THAMANI AFRIKA MASHARIKI…AZAM FC BABA LAO…

YANGA YAIPITA SIMBA KWENYE KLABU ZENYE THAMANI AFRIKA MASHARIKI…AZAM FC BABA LAO…

Yanga SC na Simba SC

Wakati mchezo wa Soka Afrika Mashariki ukizidi kushika hatamu na kuwa mchezo namba moja kwa kupendwa zaidi, vivyo hivyo klabu za ukanda huo haswa kwa nchi za Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda vinazidi kupiga hatua kubwa kimaendeleo.

Tovuti mashuhuri duniani la mambo ya thamani na masoko kwenye mchezo wa kandanda, ya ‘Transfer Market Wolrd’ imeorodhesha thamani ya sokoni kwa klabu za nchi hizo huku miamba ya soka kutoka Tanzania, Simba na Yanga zikishika nafasi ya pili na tatu.

Katika orodha hiyo, klabu nyingi za Tanzania zimechomoza kwa kuwa na thamani kubwa zaidi kuliko klabu za Uganda na Kenya.

Kinara wa Thamani kwenye ukanda huu ni Klabu cha Azam FC ambacho inakadiriwa uwekezaji wlaiofanya matokeo wanayoyapa ndio jumuisho kuu la thamani yao.

Hata hivyo, huenda kigezo cha thamani hizi pia kukaangaliwa na gharamza usajili pamoja na matumizi ya uendeshaji kwa klabu hizo.

Ifuatayo ni orodha ya klabu hizo kwa kuanzia chini kwenda juu:-

Vilabu vyenye Thamani zaidi Afrika Mashariki.

10: Gor Mahia (Kenya) – Value, $572,200

09. Tusker Fc (Kenya) – Value $596,000

08: Rayon Sport (Rwanda) – Value, $600,000

07: Singida Big Stars (Tanzania) – Value: $623,000

06: Kagera Sugar ( Tanzania) – Value $635,000

05: Mtibwa Sugar (Tanzania) – Value: $657,000

04: Vipers Fc (Uganda) – Value: $975,000

03: Simba Sc ( Tanzania) – Value: $ 2.93M

02: Yanga Sc ( Tanzania) – Value: 3: 15M

01: Azam Fc ( Tanzania) – Value: $ 6.98M

Source: Transfer Market World.

SOMA NA HII  BAADA YA MZUNGUKO WA KWANZA KUISHA...KIKOSI BORA CHA MASTAA WA NNJE HIKI HAPA...