Home Habari za Simba Leo AZIZ KI NA FEISAL KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA.

AZIZ KI NA FEISAL KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA.

Habari za Michezo

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, limetoa orodha ya wachezaji wanaowania tuzo mbalimbali katika vinyang’anyilo tofauti, huku tuzo ya mchezaji bora wa Ligi kuu ya NBC ikiwa na msisimko wake.

Tuzo hizo zitatolewa Agosti 1, katika Ukumbi wa Super Dome Masaki, siku mbili kabla ya Tamasha la Simba na Wiki ya Wananchi.

Wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa NBC Premier League ni hawa hapa:-
1. Stephane Aziz Ki,
2. Feisal Salum,
3. Kipre Jr.
4. Djigui Diarra,
5. Ley Matampi,
6. Yao Kouassi
7. Ibrahim Bacca,
8. Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr.’.

Walinda Mlango Wanaowani tuzo ya golikipa bora wa NBC Premier League ni hawa hapa:-
1. Ayoub Lakred
2. Djigui Diarra
3. Ley Matampi

Mabeki Wanaowania tuzo ya beki bora wa NBC Premier League ni hawa hapa:-
1. Yao Kouassi
2. Ibrahim Bacca
3. Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr.’

Wachezaji 3 Wanaowania tuzo ya kiungo bora wa NBC Premier League
1. Stephane Aziz Ki
2. Feisal Salum
3. Kipre Junior

Makocha Wanaowania tuzo ya kocha bora wa NBC Premier League ni hawa hapa:-
1. David Ouma,
2. Bruno Ferry,
3. Miguel Gamondi.

Huenda Stephen Aziz Akatwaa tuzo zaidi ya moja baada ya tuzo yake ya Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC, kuwa haina mpinzani.

Mbali na hayo Mchezaji  wa Azam FC Feisal Salum Feitoto anatupiwa jicho la ziada katika tuzo za msimu huu,  kwani alikuwa na msimu bora sana, akimaliza kama kinara wa ufungaji katika klabu ya Azam FC, na nyuma ya Aziz Ki kwa mabao 19.

SOMA NA HII  YANGA KULIPA KISASI SHIRIKISHO...KUCHEZA NA WABABE HAWA ROBO FAINALI