Home Habari za michezo YANGA KULIPA KISASI SHIRIKISHO…KUCHEZA NA WABABE HAWA ROBO FAINALI

YANGA KULIPA KISASI SHIRIKISHO…KUCHEZA NA WABABE HAWA ROBO FAINALI

Habari za Yanga SC

Droo ya hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho imemalizika nchini Misri kwa timu zinazowakilisha Tanzania Simba na Yanga kujua wapinzani wao.

Yanga ambayo droo yake ilianza mpinzani wake robo fainali ni Rivers United ya Nigeria ambaye alimtoa msimu uliopita katika michuano hiyo.

Mechi hiyo ambayo wachezaji wa Yanga wameiita ni ya kisasi kama itavuka hatua hiyo atakutana na mshindi wa mechi ya Pyramid FC vs Gallant na mechi hiyo itaanzia uwanja wa nyumbani Mkapa.

Mechi ya kwanza kwa Yanga dhidi ya Rivers itapigwa nchini Nigeria kati ya Aprili 21-23 na marudiano uwanja wa Mkapa Aprili 28-30.

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amesema walitamani kukutana na Rivers United timu ambayo iliwatoa msimu uliopita michuano hiyo na sasa wanakutana tena kwenye robo fainali.

Mayele amesema mechi zilizopita alikosa kucheza dhidi ya timu hiyo na sasa timu hiyo inakwenda kulipa kisasi.

“Mimi binafsi nilikuwa namtaka kwasababu mwaka jana sikupata nafasi ya kucheza naye, tulitolewa mapema watu wakaongea sana kwahiyo tumempata sehemu nzuri,” amesema Mayele

Kwa upande wa Simba SC katika Ligi ya Mabingwa itacheza dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco ikianzia uwanja wa Mkapa, Dar na kumalizia Morocco ambapo ilitoka kucheza dhidi ya Raja mechi ya mwisho hatua ya makundi ikifungwa mabao 3-1 na kuweza kupata bao katika uwanja wa Mohammed V ikiitibulia Raja ambayo haikufungwa bao katika hatua hiyo uwanja wa nyumbani.

Kama Simba ikivuka hatua ya robo atakutana na mshindi wa mechi ya Belouzdad Vs Mamelodi Sundowns.

Mechi ya kwanza itapigwa Aprili 21-22 na marudiano Aprili 28-29

SOMA NA HII  MUDA WA KUKUSANYA MAOKOTO HUU HAPA...PANGA MKEKA WAKO KAMA HIVI KISHA NISHUKURU BAADAYE...