Home Habari za michezo MECHI YA SIMBA NA YANGA MCHEZAJI AFARIKI UWANJANI…TUKIO HILI LINASIKITISHA SANA!

MECHI YA SIMBA NA YANGA MCHEZAJI AFARIKI UWANJANI…TUKIO HILI LINASIKITISHA SANA!

MECHI YA SIMBA NA YANGA MCHEZAJI AFARIKI UWANJANI...TUKIO HILI LINASIKITISHA SANA!

Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Songwe (SODIFA) kimetangaza kifo cha mchezaji wa timu ya Saza FC, Albat Andrea aliyefariki baada ya kugongana na mwenzake katika kuwania mpira.

Tukio hilo limetokea katika mchezo wa kirafiki kati ya mashabiki wa Yanga na Simba wakichuana katika kusheherekea Sikukuu ya Pasaka.

Andrea aliyekuwa anacheza nafasi ya kiungo alifariki dunia njiani wakati anakimbizwa hospitali kupatiwa matibabu.

Ofisa Habari Chama cha Soka Mkoa wa Songwe (SOREFA), Charles Mwamlima, amethibitisha taarifa hiyo huku ikielezwa taratibu za kusafirishwa mwili wa marehemu kuelekea Geita zinafanyika.

SOMA NA HII  KLABU YA SIMBA YAONDOLEWA KATIKA MASHINDANO YA LIGI KUU, ISHU IKO HIVI