Home Uncategorized WACHEZAJI YANGA KULA CHRISTMAS MBEYA

WACHEZAJI YANGA KULA CHRISTMAS MBEYA


VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kwa sasa wapo Mbeya wakiendelea kuivutia kasi Klabu ya Tanzania Prisons.

Yanga inakula Christimas ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 17 na kibindoni ina jumla ya pointi 43.


Imecheza mechi zote 17 mfululizo kwa msimu wa 2020/21 kwenye raundi ya kwanza bila kupoteza baada ya kumalizana na Ihefu na kushinda mabao 3-0.


Ilipaswa Jumamosi, Desemba 26 imenyane na  Singida United mchezo wa hatua ya tatu Kombe la Shirikisho Afrika ila kutokana na timu ya Singida Unite kushushwa madaraja mawili kwa kushindwa kufika kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Alliance wanapenya hatua ya nne.


Meneja wa Klabu ya Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa kwa sasa wachezaji watarejea kuanza mazoezi rasmi Desemba 26.Leo wachezaji wote ikiwa ni pamoja na ingizo lao jipya, Saido Ntibanzokiza watakuwa huru 


 “Desemba 26 wachezaji wataanza kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo wetu wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.


“Wachezaji wapo huru tutakutana Jumamosi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo wetu utakuwa Uwanja wa Nelson Mandela hivyo utaratibu wa safari utawekwa wazi hivi karibuni,” .


Mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Tanzania Prisons iligawana pointi moja na Yanga, hivyo mchezo huu utakuwa ni wa kisasi kwa timu zote mbili.

Kila timu itakuwa inahitaji kusepa na pointi tatu ambapo kwa Prisons wao watapambana kuvunja rekodi ya Yanga kutofungwa na Yanga watapambana kuifunga Prisons ambayo iliwatungua bao 1-0 wapinzani wao Simba.
SOMA NA HII  SIMBA YAIDAI MABAO 20 MTIBWA SUGAR FC