Home Habari za michezo KLABU YA SIMBA YAONDOLEWA KATIKA MASHINDANO YA LIGI KUU, ISHU IKO HIVI

KLABU YA SIMBA YAONDOLEWA KATIKA MASHINDANO YA LIGI KUU, ISHU IKO HIVI

Kikosi cha Simba Msimu huu 23/24

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almasi Kasongo amesema waandaaji wa mashindano ya Super League wameomba klabu ya Simba itolewe kwenye ratiba ya Ligi Kuu Bara kuanzia Oktoba 20 hadi Novemba 21 kwa ajili mashindano ya kimataifa ya African Super League.

Almasi aliyasema hayo jana Agosti 7, 2023 alipokuwa akitangaza ratiba ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023-24.

“Wameomba na ndio maana unaona michezo yao katika kipindi hicho tumeiwekea TBA, hivyo michezo yao watakuja kuicheza pale nafasi itakapopatikana,” alisema Kasongo.

Hivyo Simba, watasimama kwa takriban mwezi mzima kwenye Ligi Kuu isipokuwa mchezo mmoja wa dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga (Novemba 5) ambao kwa mujibu wa Kasongo, umeachwa tarehe hiyo mpaka pale Shirikisho la Mpira Afrika watakaposema vinginevyo.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA KUUNGANA NA GSM YANGA....MANJI KAVUNJA UKIMYA...JIBU LAKE HILI HAPA...