Home Uncategorized COASTAL UNION YATAJA SABABU YA KUFUNGWA MABAO 7-0 NA SIMBA

COASTAL UNION YATAJA SABABU YA KUFUNGWA MABAO 7-0 NA SIMBA


 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa hawezi kubadilisha matokeo aliyoyapata kwa timu yake kufungwa mabao 7-0 dhidi ya Simba kwa kuwa yameshatokea kutokana na makosa ya kujirudia kwa wachezaji wake ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.


Coastal Union inaweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kwa msimu wa 2020/21 kufungwa mabao mengi bila safu yake ya ushambuliaji kuambulia bao kwa kuwa timu ya kwanza iliyofungwa mabao mengi ilikuwa ni Mwadui FC iliyofungwa mabao 6-1 na JKT Tanzania.


Mabao kwa upande wa Simba yalifungwa na Hassan Dilunga ambaye bao lake lilileta utata kutoka kwa wachezaji wa Coastal Union ambao walionekana kumfuata mwamuzi wa kati wakidai kwamba mfungaji na mtoa pasi John Bocco walikuwa wameotea.


Mabao mengine yalifungwa na John Bocco ambaye alifunga hat trick yake ya kwanza ndani ya Simba ikiwa ni ya pili kwenye ligi kwa kuwa wa kwanza kufunga alikuwa ni Adam Adam wa JKT Tanzania na mengine yalifungwa na Clatous Chama aliyefunga mawili na Bernard Morrison alifunga bao moja.


Mgunda amesema:”Hakuna namna ya kufanya kwa kuwa matokeo yameshatokea siwezi kuyabadili na nimekubali nimepoteza hivyo makosa yaliyotokea tutayafanyia kazi.


“Tumefungwa kwa sababu ya makosa ya kujirudiarudia kwa wachezaji hasa kipindi cha kwanza tukafungwa mabao mengi ila angalau kipindi cha pili makosa yalipungua, tumefungwa kwa sababu ya makosa yetu hakuna namna tutafanyia kazi makosa, matokeo hatuwezi kuyabadili,” amesema.

SOMA NA HII  HAYA HAPA MAJEMBE SABA YA KAZI AMBAYO YAMEMALIZANA NA YANGA