Home Uncategorized NYUMA YA JONAS MKUDE KUKOSEKANA KIKOSINI SABABU NI UTOVU WA NIDHAMU

NYUMA YA JONAS MKUDE KUKOSEKANA KIKOSINI SABABU NI UTOVU WA NIDHAMU

 


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa sababu kubwa iliyofanya kiungo wake namba moja ndani ya Simba, Jonas Mkude kukosa mchezo wa jana Novemba 21 dhidi ya Coastal Union ni kuchelewa kuripoti kambini.


Jana Coastal Union ilikubali kufungwa mabao 7-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na Simba huku Mkude akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliokosa mchezo huo. 


Wengine wa Simba ambao walikosa mchezo huo ni pamoja na Luis Miquissone na Meddie Kagere waliochelewa kuripoti kambini kutokana na kuwa kwenye timu zao za Taifa na Chris Mugalu na Gerson Fraga ambao ni majeruhi.


Sven amesema:” Mkude alichelewa kurudi kambini baada ya kutoka kwenye timu ya taifa wakati wenzake wakiwa wamerejea kwa wakati sahihi.


“Kwa hiyo mechi dhidi ya Coastal Union alikuwa na adhabu ya kinidhamu ya kuukosa mchezo huo kutokana na suala hilo la nidhamu ambalo amelifanya,”.

Simba imefikisha jumla ya pointi 23 ikiwa nafasi ya tatu na vinara wa ligi ni Azam FC wenye pointi 25 huku wakifuatiwa na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 24.

SOMA NA HII  POGBA: SIPENDI KUONA LIVERPOOL IKITWAA UBINGWA, TULISTAHILI SISI KUUBEBA