Home Yanga SC MASHINE MPYA YA YANGA KAMILI GADO KUANZA KAZI

MASHINE MPYA YA YANGA KAMILI GADO KUANZA KAZI


BEKI mpya wa Klabu ya Yanga, Dickson Job ametamba kuwa sasa yupo fiti baada ya kupona majeraha ya misuli yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Job aliyesajiliwa kutoka ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar amekuwa nje ya uwanja tangu mwezi Januari mwaka huu baada ya kupata majeraha hayo akiwa kwenye kambi ya kikosi cha timu ya Taifa, iliyokuwa ikijiandaa na michuano ya CHAN iliyofanyika nchini Cameroon mwanzoni mwa mwaka huu.

Job amesajiliwa na Yanga akitokea Mtibwa Sugar aliyoichezea tangu mwaka 2016, katika kipindi cha dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15, mwaka huu.

Akizungumzia maendeleo yake Job amesema: “Kwa sasa naendelea vizuri baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya misuli.

“Nimeanza mazoezi na timu na ni faraja kwangu kurejea tena uwanjani kwa ajili ya kuisaidia timu yangu,”. 

Ataungana na mabeki wengine wa kati ambao ni Bakari Mwamnyeto, Lamine Moro, Said Juma na Abdalah Shaibu kuweka ngome ya kikosi salama.


 

SOMA NA HII  KISINDA NI MCHEZAJI HALALI WA YANGA, MKWANJA WATAGAWANA NA AS MANIEMA