Home Habari za michezo KISA YANGA KUTINGA FAINAL CAF….WACHINA BONGO WATOA TAMKO LAO…

KISA YANGA KUTINGA FAINAL CAF….WACHINA BONGO WATOA TAMKO LAO…

Habari za Yanga SC

Yanga imeendelea kupokea salamu za pongezi ambapo China nayo imetoa pongezi zake kufuatia timu hiyo kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Salamu za China zimetolewa na Balozi wao wa nchini Tanzania Chen Mingjian kupitia ukurasa wake wa Twitter akiwapongeza Yanga kwa kufika hatua hiyo ya kihistoria.

Sambamba na salamu hizo Balozi Mingjian amewataka Yanga kujitahidi katika mechi za fainali watakapokutana na USM Alger ya Algeria.

Baada ya salamu hizo naye Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amemshukuru Balozi Mingjian huku akisema hatua hiyo imetokana na jitihada na mapambano ya klabu yao.

“Hii inaonesha namna watu wa Jamhuri ya China mmejawa na utu,uhusiano wa China na Tanzania ni wa kipekee,”ameandika Arafat.

Aidha Arafat amemkaribisha Balozi Mingjian kwa mualiko maalum kwenye mchezo wa kwanza wa fainali utakaopigwa Mei 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga imefuzu fainali baada ya kuwang’oa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-1 wakishinda nyumbani za ugenini

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA WACHEZAJI WA MBEYA KWANZA WALIVYO...MAKATA KAGUNA..KISHA AKASEMA HAYA...