Home Habari za michezo ROBERTINHO ANAVYOPITA KWENYE MIFUMO YA GAMONDI

ROBERTINHO ANAVYOPITA KWENYE MIFUMO YA GAMONDI

Habari za Simba leo

Juzi kocha wa Yanga alilazimika kumpanga Gift Mauya badala Khalid Aucho katika kiungo cha chini. Doctor Aucho ndiye mchezaji muhimu zaidi Yanga, tayari ana kadi mbili za njano na kama jana angeona kadi nyingine basi angewakosa Simba.

Pacha wake katika kiungo, Mudathir Yahya na yeye ilibidi aende benchi mapema ili kumuweka fiti kwa ajili ya mechi ijayo. Kama ilivyo kwa Aucho, unamuhitaji Mudathir bora wakati wote ili kiungo cha Yanga kisogee.

Baada ya kuongoza mabao mawili Yanga waliamua kupunguza kasi ya mchezo. Wakajihami kwa kumiliki mpira, wakapunguza kukimbia ili kutunza nguvu kwa ajili ya mechi ijayo. Kumbuka bado walikuwa na ratiba ngumu sana hadi kufika juzi.

Kama ilivyo kwa Yanga, Simba wamecheza mechi ngumu mfululizo na wametumia nguvu kubwa. Mbaya zaidi hawajapata nafasi ya kubadilisha/kuwapumzisha wachezaji wao wengi.

Ni Henock Inonga pekee ambaye hajacheza ‘panga pangua’ katika kikosi cha Simba na ni kwa sababu ya majeraha.

SOMA NA HII  SIMBA SC IMEPANIA KURUDISHA UFALME WAKE BAADA YA KUKOSA MATAJI.... LEO KLABU YA SIMBA IMEMTANGAZA MCHEZAJI WAKE HUYU MPYA