Home Habari za michezo TRY AGAIN:- BAADA YA KUMALIZANA NA MBABE WAO JANA….KINACHOFUATA NI WAO SASA...

TRY AGAIN:- BAADA YA KUMALIZANA NA MBABE WAO JANA….KINACHOFUATA NI WAO SASA KULIA…

Habari za Simba

BAADA ya kufanikiwa kuvuna pointi tatu dhidi ya Ihefu FC, uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa mechi hiyo ilikuwa sehemu ya maandalizi kwa mchezo ujao wa dabi na ushindi walioupata ni salaam kuelekea mchezo wa watani wa jadi, Yanga.

Umesema licha ya ubora wa Yanga lakini hawana kitu kingine zaidi ya ushindi kwani ndicho kitu pekee kitachowapeleka kwenye ramani za mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba imeendelea kupata ushindi katika mchezo wake wa sita jana kwa kuifunga Ihefu FC mabao 2-1, uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam ukiwa ni ushindi wa asilimia 100, ikiwa bado siku sita ya Darby ya Kariakoo inayotarajiwa kuchezwa Novemba 5, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, alisema japo wachezaji walikuwa na uchovu, vijana walitumia walicheza kwa mipango licha ya kutafuta ushindi lakini benchi la ufundi walitumia kama sehemu ya maandalizi ya mechi yetu ijayo dhidi ya Yanga.

“Challenge ipo ligi ngumu kila timu imejipanga , inakuja kivingine na kubalidilika ni jambo jema kwa sababu inaonyesha ubora wa ligi yetu, hatukutarajia kuona Namungo FC anashinda dhidi ya Azam FC.

Sisi Simba tunaenda kwa mipango hatutaki kukurupuka kila mechi unaingia na mbinu zake tukishinda moja sawa kikubwa na alama tatu. Hii mechi ya leo (juzi) imekuwa sehemu ya kujiandaa na Darby dhidi ya watani wetu,” alisema Try Again.

Aliongeza kuwa Darby ya Kariakoo ni mechi kubwa wanaiheshimu inatenda haki kutoa lamani ya ubingwa, wako makini kwa mechi kubwa na ngumu ambaye atacheza vizuri atapata matokeo mazuri.

“Wapinzani wetu wako vizuri wachezaji wanapambana na wanajituma kutafuta ushindi, Simba tumejipanga vizuri na itakuwa mechi ya burudani kwa mashabiki wetu, wasije kusahau ni mechi yetu tuko nyumbani.

Niwaombe wanasimba wajitokeze kwa wingi robo tatu ya uwanja iwe nyeupe na nyekundu ili wachezaji wetu wapata nguvu na kuona sapoti kubwa kuliko mechi za awali,” alisema Mwenyekiti huyo.

Alisisitiza kuwa wamejipanga vizuri dhidi ya Yanga na tayari uongozi umeweka mikakati yake kuelekea mchezo huo ambao wamefanikiwa kutoa ahadi kwa wachezaji wao endapo watashinda mchezo huo.

“Hatuwezi kuweka siraha zetu hadharani ila tumejipanga vizuri. Huwezi kusema kiti kuhusu ubingwa kwa mechi sita wakati kuna michezo 30 mbele , mapema sana licha ya nia yetu ni hiyo.

Ligi ni ngumu na chochote kinaweza kutokea unaweza kushinda kwenye mechi kubwa ukapoteza ndogo pia ukapoteza na kushinda kubwa.

Kwa mechi hizi sita sitaweza kusema tayari tupo kwe njia ubingwa kama unaenda Morogoro basi tuko Ubungo, wachezaji waongeze bidii kwa sababu wanasimba wanatamani kuona makubwa zaidi ya yale wanayoyaina sasa,” alisema Try Again.

Alisema ukilinganisha na timu imetoka katika mashindano makubwa ya Afrika Football League (AFL), sasa wanaelekea ligi ya Mabingwa Afrika, wanatamani kuona makosa yaliyojitokeza nyuma hayatokei tena.

“Wachezaji na benchi la ufundi wanasimba wamechoka kusubiri wanataka kuona timu ikifanikiwa kila wakati na kwenda mbele zaidi,” alisema Mwenyekiti huyo.

SOMA NA HII  UKIACHA MAMBO MENGINE 'MEUSI'...HIZI HAPA SABABU ZA CAF KUITEMA BIASHARA ...TFF WATIA NENO..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here