Home Habari za michezo RAIS WA FIFA NA CAF KUZISHUHUDIA SIMBA NA YANGA KESHO KUTWA….MAJALIWA AWAOA...

RAIS WA FIFA NA CAF KUZISHUHUDIA SIMBA NA YANGA KESHO KUTWA….MAJALIWA AWAOA NENO LA KUZINGATIA…


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa amewaomba Rais wa Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’ Gianni Infantino na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ Patrice Motsepe kuwa sehemu ya watakaoshuhudia mchezo wa Kuwania Ngao ya Jamii, Jumamosi (Agosti 13), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mabingwa wa Tanzania Bara Young Africans watacheza dhidi ya Simba SC katika mchezo huo, ambao utatumika kama kiashirio cha kufunguliwa kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23.

Waziri Mkuu Majaliwa amewaomba viongozi hao, akiwa mjini Arusha katika Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’, ambapo Tanzania imebahatika kuwa mwenyeji kwa mara ya kwanza.

Waziri Mkuu pia amewaomba Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ‘CAF’ kufika Dar es salaam kutazama mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Tanzania.

“Simba, Young Africans na Azam FC ni vielelezo vya soka la Tanzania. Naomba tarehe 13 mje uwanja wa Mkapa kutazama Derby ya Kariakoo ambapo ni Derby kubwa na yenye mvuto barani Afrika” amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Msimu uliopita Simba SC ilipoteza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Young Africans kwa kufungwa 1-0, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, bao likifungwa na Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Mayele.

SOMA NA HII  WAKATI WAKIINGIA KAMBINI JANA...MATOLA AFUNGUKA NA KUANIKA UDHAIFU WA SIMBA...CAF KAMA KAWA...