Rashfod ambaye ni mshambuliaji pia wa timu ya taifa ya England ametunukiwa udaktari Oktoba 7 kwenye hafla iliyofanyika Old Trafford na kuwa miongoni mwa vijana wachache waliotunukiwa wakiwa katika umri mdogo wa miaka 23 kwa historia ya chuo hicho.
Ikumbukwe kwamba hafla hiyo ilipaswa kufanyika Julai mwaka uliopita ila ilishindikana kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Katika hafla hiyo iliweza kuhudhuriwa na familia yake pamoja na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Sir Alex Ferguson ambaye alishawahi kutunukiwa tuzo hiyo ya heshima kutoka Chuo cha Manchester.
Katika hotuba yake baada ya kutunukiwa tuzo hiyo ya heshima, Rashford alitumia hotuba yake katika sherehe hiyo kuwasihi wanasiasa kujitokeza katika jamii kama mji wake ili kusaidia watoto na familia zinazoishi mazingira hatarishi.
Pia amesema kuwa ni furaha kwake kuweza kupewa tuzo hiyo mbele ya wale ambao ni mfano kwake katika maisha ya kazi yake ya mpira.
“Kuwa hapa na uwepo wa watu wakubwa kama Sir Alex na wote ambao wamekuwa bega kwa bega nami kwenye safari yangu ambayo nipo hapa ni kitu cha upekee mkubwa.
“Nipo hapa kupokea tuzo yangu ya heshima katika udaktari kwa ajili ya kazi yangu ya inayowahusu watoto na umasikini. Jana, mamilioni ya familia kuizunguka Uingereza wameweza kupoteza wale ambao walikuwa wakiwategemea hivyo wanakuwa bila msaada a suala la umasikini linazidi kuongezeka kutoka kwa mtoto mmoja mpaka watato watatu bado hali ni ngumu.
“Kwa sasa ni muhimu kila mmoja kupambana na kufanya kama vile ambavyo ninafanya, ni wakati wakuona harakati zinaendelea. COVID 19 isiwe sababu ya kufanya watu wasiweze kupambana na kusaidia wengine,” .