Home news TAIFA STARS YAKWEA PIPA KUWAFUATA BENIN

TAIFA STARS YAKWEA PIPA KUWAFUATA BENIN


WACHEZAJI wa timu ya Tanzania, Taifa Stars wakiwa katika ndege ya Air Tanzania aina ya Airbus A220-300 tayari kwa safari ya Benin ambayo itachukua saa 5:20.

Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen ina kibarua cha kwenda kusaka pointi tatu mbele ya Benin kwa ajili ya kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia Qatar 2022.

Katika mchezo uliochezwa jana Oktoba 7, Stars ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 hivyo ina kibarua kizito cha kusaka ushindi ugenini.

Poulsen amesema kuwa anawaamini vijana wake wanaweza kupata matokeo kwenye mchezo huo kwa kuwa makosa ambayo wameyafanya watayafanyia kazi.

“Makosa ambayo tumeyafanya kwenye mchezo wa mwanzo tutayafanyia kazi ili kuweza kupata ushindi kwenye mchezo wetu wa marudio.

“Vijana walikuwa wanahitaji ushindi ila walikwama kumalizia nafasi ambazo walitengeneza hivyo bado tuna muda wa kufanya kwenye mechi ijayo,” .


SOMA NA HII  MORRISON AIBUA JIPYA AKIWAGA WENZAKE KAMBINI...KAKUSANYA MPAKA MASHUKA...MZAMIRU AMTUPA YANGA...