Home news SIMBA YAKATAA MATOKEO YA MECHI YA NGAO YA JAMII KWA MKAPA

SIMBA YAKATAA MATOKEO YA MECHI YA NGAO YA JAMII KWA MKAPA


BAADA ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Simba wamebainisha kuwa hawakustahili matokeo hayo.

Kwa ujumbe huo ni kama wameyakataa matokeo hayo kwa kuwa walikuwa na nia ya kutwaa tena Ngao ya Jamii ila mambo yalikuwa magumu kwao ndani ya uwanja.

Bao pekee la Yanga lilipachikwa na Fiston Mayele kwa shuti kali lililomshinda Aishi Manula ambaye hakuwa na chaguo dakika ya 10 ya mchezo katika Uwanja wa Mkapa.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba, mabosi hao ambao walikuwa wanaitetea Ngao ya Jamii waliandika kwamba, “Hatukustahili matokeo haya,!”

SOMA NA HII  SIMBA KUTWA MARA MBILI, WACHEZA MECHI ZA KIRAFIKI